Baada ya kuenea kwa uvumi kwamba viongozi
wa Yanga SC wakati wowote watamfuta kazi Kocha wao Raia wa Tunisia Nassredine
Nabi kwa madai kadhaa, CEO wa Yanga SC Andre Mtine amekanusha uvumi huo na
kusema Nabi bado yupo Yanga Sc.
“Niwaombe washabiki na wanachama wetu kuwa
na utaratibu wa kufuatilia taarifa za club yetu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya
habari, tuna Yanga App na website ambazo zimekuwa zikitoa taarifa zetu kwa
usahihi”>>> Andre Mtine
Mengi yanasemwa kuhusiana uvumi huo lakini awali zilidaiwa kuwa Nabi atafutwa kazi kutokana na kutosikiliza ushauri wa wenzake wa benchi la ufundi sambamba na kutokubaliana na baadhi ya sajili za wachezaji wapya Yanga Sc wakati wa usajili.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka ZaidiDownload/Pakua App ya Timu ya Wananchi Google Playstore BOFYA HAPA
Tags
Habari