NI yule yule Fiston Mayele ambaye alitoka kuiadhibu Singida BS ndiye aliyezamisha jahazi la Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Liti na kuifanya Yanga Sc irejee kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara huku wakiishusha Azam kwenye nafasi hiyo wote wakiwa na alama 29, wametenganishwa na mabao.
Yanga Sc ambayo ilitembeza boli na kuwaacha na furaha
mashabiki zao ambao walijitokeza kwa wingi uwanjani hapo, imerejea kileleni huku wakiwa na mchezo mmoja
mkononi tofauti na wenzao, Azam FC.
Hizi ni dondoo muhimu
kuhusu mchezo huo wa Ligi ambao Yanga Sc iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yote
yakifungwa na Mayele.
Ulikuwa ushindi wa nne
mfululizo kwa Yanga Sc tangu mara ya mwisho kutoka sare ya bao 1-1 kwenye
mchezo wa watani wa jadi.
Ulikuwa mchezo wa pili
mfululizo kwenye ligi kwa Abutwalib Mshery kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga Sc.
Mabao mawili ambayo alifunga
Mayele yanamfanya kuwa kinara wa mabao Ligi Kuu Bara akiwa na mabao manane.
Kilikuwa kipigo cha
nne kwa Dodoma Jiji kutoka kwa Yanga Sc ndani ya michezo mitano tangu kupanda kwao ligi kuu, wamekuwa vibonde
kwa mabingwa hao wa Kihistoria.
Yanga Sc imeendeleza rekodi yao ya kucheza michezo mfululizo (48) kwenye ligi bila ya kupoteza, anayefuata kwenye ratiba yao ni Mbeya City
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka Zaidi