Timu ya Wananchi,
Yanga Sc wameandika historia kwa kupata ushindi ugenini
na kutinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Ushindi pekee umepatikana kipindi cha pili
kupitia kwa kiungo wa Yanga Aziz KI ambaye alianzia benchi kwenye mchezo wa
leo.
Dakika 45 za awali ni beki Kibwana Shomar
alikuwa ni mwiba kwa wapinzani wao Club Africain ambapo alipiga mashuti mawili
ambayo yalilenga lango.
Kiungo Bernard Morrison na Sure Boy
walikuwa na kazi kubwa uchezesha timu ya Yanga iliyocheza soka la pasi nyingi
kipindi cha kwanza na cha pili.
Bao la ushindi limepachikwa dakika ya 79
kwa nyota huyo kuwatungua Waarabu wa Tunisia kwa shuti lilimshinda mlinda
mlango.
Pongezi kwa kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui ambaye alifanya kazi kubwa kuweka lango salama dakika.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka ZaidiDownload/Pakua App ya Timu ya Wananchi Google Playstore BOFYA HAPA
Tags
Kimataifa