Mchezo huo wa raundi
ya 11 utachezwa Novemba 13 utakuwa wa tano wa nyumbani kwa Kagera Sugar kwenye
uwanja huo huku mmoja pekee ukipigwa Kaitaba dhidi ya Singida Big Stars ambao
ilicheza bila mashabiki.
Katibu wa Kagera
Sugar, Ally Masoud, alisema sababu kubwa ya kupeleka mchezo huo Mwanza ni
kutokukamilika kwa uwanja wao huku kikosi kikijifua mjini Bukoba kwa maandalizi
ya mchezo huo.Katibu wa Chama cha Soka mkoa wa Kagera (KRFA), Al-amin Abdul
alisema wamefuatilia matumizi ya fedha hizo na utekelezaji wa mradi lakini
manispaa imekuwa ikitoa majibu yasiyoeleweka ambapo amejivua lawama na
kuwatupia zigo hilo.
Akitolea ufafanuzi wa
madai hayo, Afisa Michezo na Utamaduni Manispaa ya Bukoba, Cletus Mutakyawa,
alikiri Kagera Sugar kutoa fedha kwa ajili ya kuharakisha uwekaji wa uzio ambao
uliondolewa wakati wa sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru Oktoba 14 mwaka huu.
Alisema fedha hizo
(akigoma kutaja kiasi) ziliwekwa na Kagera Sugar kwa makubaliano maalum na
Manispaa ya Bukoba kuwa baadae zitarejeshwa kwani ilikuwa ni dharura
kuharakisha ukarabati huo huku akisisitiza kuwa matumizi ya fedha hizo lazima
yafuate taratibu za Serikali.
Hata hivyo alieleza
kuwa ujenzi wa uzio huo umeshakamilika siku tatu zilizopita na tayari Bodi ya
Ligi imejulishwa.
“Wao wakati wanapiga
kelele sisi tayari tulikuwa tumeanza kazi na uzio umekamilika tangu juzi na tumewatumia
picha. Ni kweli fedha zilitolewa na Kagera Sugar lakini zitarudishwa.”