AZIZ KI nyota wa Yanga Sc atakosekana kwenye mechi tatu zinazofuata kwa timu yake hiyo msimu wa 2022/23.
Sababu ya nyota huyo kukosekana kwenye
mechi hizo ni maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania ambayo yametolewa kutokana na kikao cha Novemba 4,2022.
Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 8,2022
ambapo kwa sasa Yanga ipo nchini Tunisia kwa ajili ya maandaizi ya mchezo wao
dhidi ya Club Africain ya Tunisia.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa nyota huyo
kwenye mchezo uliochezwa Oktoba 23,2022 alifanya kosa la kukwepa kusalimiana na
wachezaji timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliokamilika kwa sare ya
kufungana bao 1-1.
Mbali na adhabu hiyo ya kukosa mechi tatu pia ametozwa faini ya laki tano.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka ZaidiDownload/Pakua App ya Timu ya Wananchi Google Playstore BOFYA HAPA
Tags
Habari