Kikosi cha Yanga Sc kina kibarua cha
kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain
kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa kesho Novemba 9,2022.
Tayari kikosi hicho kipo nchini Tunisia kwa
ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao utaamua nani atasonga mbele
kwenye hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho.
Mayele amesema:”Hatujawahi nchini Tunisia
kwa ajili ya kuona tunapoteza mchezo wetu bali tunahitaji kupata matokeo mazuri
na inawezekana mashabiki wawe pamoja nasi,” amesema.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja
wa Mkapa ubao ulisoma Yanga Sc 0-0 Club Africain.
Ikumbukwe kwamba Novemba 4,2022 kikosi cha Yanga Sc kilisepa Dar kwa kupitia Dubai kisha kikaibuka nchini Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa kimataifa.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka Zaidi