Hersi: Hatua ya Makundi Shirikisho lazima..

MWANZA. Rais wa Yanga Sc, Hersi Said amewahakikishia mashabiki, wanachama na wapenzi wa Timu ya Wananchi, Yanga Sc, itafuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Club Africain ya Tunisia baada ya kukwama Ligi ya Mabingwa.

Yanga Sc itaanzia nyumbani Novemba 2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ikiwakaribisha Club Africain mchezo wa mtoano kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.

Akizungumza jijini Mwanza juzi Ijumaa na viongozi na wanachama wa matawi zaidi ya 25 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, Hersi alisema uongozi umejiandaa kuhakikisha wanasonga mbele huku akiwatahadharisha mashabiki na wanachama wa timu hiyo kujiandaa kwa lolote na wasipende kulaumu pale timu inapoteleza.

Alisema mashabiki wanapaswa kuwa nyuma ya timu wakati wote bila kuwa sehemu ya wanaoibomoa na kuikana pale inapofungwa, huku akisisitiza ushindi kwenye mechi yao ya ligi utawapa hali ya kujiamini kuelekea mchezo huo.

“Nataka niwahakikishie tutasonga mbele kwenda hatua ya makundi, siyo jambo baya kuumia kwa kitu unachokipenda, lakini usiipende Yanga Sc kisa inashinda ikifungwa siyo yako. umeipenda nembo ya Yanga, rangi na klabu, hujaipenda sababu ya matokeo, sisi tunapaswa kuwa na mapenzi na klabu hii na siyo mapenzi na matokeo, kama ni hivyo katafute kitu kingine cha kupenda.”

“Hili tatizo la kuipenda timu ikishinda tuachane nalo na watu kama hao siyo wana Yanga. Mfano Barcelona na Manchester United mara ya mwisho wamechukua ubingwa lini licha ya uwekezaji unaofanywa? Lakini kila siku wako nyuma ya timu yao,” >>alisema Hersi ambaye alitumia jukwaa hilo kuwashukuru wanachama kwa kumchagua kuwa Rais.

Kwa upande wake, Afisa Habari wa Yanga Sc, Ali Kamwe alisema kama watashinda dhidi ya Geita Gold Fc na kukaa kileleni itawajengea wachezaji na viongozi hali ya kujiamini dhidi ya Club Africain kwani wamejipanga vyema kuwakabili waarabu hao. “Uhitaji wa alama tatu kwenye mechi zilizo mbele yetu ni muhimu tukianza na Geita Gold ni mchezo muhimu na ushindi utatujengea confidence,” alisema.

TAZAMA BAO LA USHINDI LA FISTON MAYELE DHIDI YA AZAM FC

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka Zaidi

Download/Pakua App ya Timu ya Wananchi Google Playstore BOFYA HAPA

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form