Kaseja aliyetamba kwa
jina la ‘Tanzania One’ ametangaza maamuzi hayo, baada ya kukosa nafasi ya
kusajiliwa kwenye klabu za Ligi Kuu msimu huu 2022/23, akiachana na KMC FC
iliyoitumikia kwa misimu miwili mfululizo.
Mkongwe huyo amesema
amechukua maamuzi ya kustaafu soka la ushindani baada ya kuona anahitaji muda
wa kupumzika, lakini amesisitiza ataendelea kuonekana katika medani ya soka
katika nyanja mbalimbali.
“Bado nina uwezo wa kucheza michezo ya ushindani na kufanya vizuri lakini kwa sasa nimeamua kupumzika.”
“Pamoja na kuacha kucheza michezo ya kiushindani kwa sasa nitaendelea kuwa kwenye familia ya soka na kufanya majukumu mengine, pia nitakapohitaji kucheza nitacheza tu, kwani bado nipo ‘FIT’.” amesema Kipa huyo
Kasema ametwaa mataji
saba ya Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na Klabu ya Simba SC katika misimu ya
2003, 2004, 2007 (Ligi Ndogo), 2010 na 212.
Pia amewahi kutwaa
mataji mawili ya Michuano ya Tusker ‘TUSKER CUP’ mwaka 2003 na 2005.
Akiwa Young Africans
aliwahi kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara mara moja, msimu wa 2008/09 na kuwa
Mlinda Lango mwenye mafanikio zaidi nchini Tanzania.
Kaseja alianza
kuonekana katika soka la ushindani mwaka 2000 akiitumikia klabu ya Moro United
aliyojiunga nayo ikiwa Ligi Kuu Tanzania Bara, akitokea Shule ya Sekondari ya
Makongo na kucheza kwa msimu mmoja, kisha kujiunga na Simba SC aliyoitumikia
kwa mafanikio makubwa zaidi kwa miaka 10.
Kaseja pia aliwahi
kuitumikia Young Africans katika vpindi tofauti kama ilivyo kwa Simba SC na
baadae alijiunga na Kagera Sugar, kisha Mbeya City na kumalizia soka lake KMC FC
mwishoni mwa msimu uliopoita.
Kwa sasa Kaseja ni
sehemu ya jopo la makocha wanaounda Benchi la Ufundi la muda la Timu ya Taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars’ chini ya Mzambia Honour Janza akisaidiana na Mzawa
Mecky Mexime