Yanga Sc wanatarajiwa
kukutana na Club Africain Novemba 2 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la
Shirikisho Afrika kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo, kwenye
Uwanja wa Mkapa, Dar.
CEO wa Yanga Sc, Andre Mtine, amesema kuwa
katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa elimu juu ya magonjwa ya Uviko-19,
watatoa chanjo kwa mashabiki 10,000 ambao watachanjwa, hivyo jambo hilo kwao
wanafanya kama sehemu ya kuelimisha jamii.
“Ushirika wetu na UNICEF kuhusu Uviko-19 na virusi vya Ebola umeanza kazi rasmi ambapo tunatoa zawadi ya tiketi 10,000 kwa mashabiki ambao watachanja chanjo ya Uviko-19 kushuhudia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa tarehe 2 mwezi ujao,” >>amesema.
Kwa upande wa Ofisa
Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema:“Kila mmoja wetu anafahamu madhara ya
Uviko-19, hivyo kupambana na Uviko-19 ni jukumu letu sote. Sisi kama Klabu
tunatamani mitaa iwe salama.
“Hatuwezi kutoa
burudani kama hatutoi elimu ya afya. Tumeandaa vitu mbalimbali, na utakutana na
viongozi mbalimbali wa klabu yetu ambao watakuja kutoa hamasa. Mayele, Feisal
na Aziz Ki pamoja na wachezaji wengine watakuwepo mitaani kutoa elimu hiyo na
kuhamasisha” >>amesema Kamwe.