Ulikuwa ni mchezo wazi kwa timu zote mbili
ambazo zilikuwa kwenye msako wa ushindi kupiga hatua moja kuelekea kwenye hatua
ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.
Kete ya kwanza ya Kocha Mkuu wa Yanga Sc, Nasreddine Nabi
imekamilisha dakika 90 za awali bilakuambulia bao ikiwa nyumbani na mashabiki
wake.
Kazi iliyopo mbele ni kusaka ushindi
ugenini nchini Tunisia mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa
utaamua hatma ya nani atakayesonga mbele.
Nyota wa Yanga, Khalid Aucho, Bernard
Morrison na Fiston Mayele ni miongoni mwa wale ambao walianza kikosi cha
kwanza.
Kwa upande wa mapigo ya mipira iliyokufa
jukumu hilo lilikuwa kwenye miguu ya Aziz KI ambaye naye alikwama kujaza mpira
nyavuni.
Mchezo huo wa marudio unatarajiwa kuchezwa
Jumatano ya Novema 9, 2022.