Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara,
licha ya kumuengua Yacouba katika orodha ya mastaa wao msimu huu, bado wapo
naye kikosini ambapo anafanya mazoezi na akiendelea kuonyesha kiwango bora
kumshawishi kocha Nabi.
Ukiachana na Yacouba ambaye sifa yake ni
kasi, lakini Mzambia Lazarous Kambole aliyesajiliwa hivi karibuni ameondolewa
kwenye usajili kumpisha Tuisila Kisinda anayetarajiwa kutua muda wowote na
klabu itaendelea kuwa nae na kumlipa stahiki zote lakini hatatumika kwani Yanga
tayari ina wachezaji 12 wa kigeni.
Kambole ambaye amesajiliwa kutoka Kaizer
Chiefs hajapata nafasi ya kuitumikia timu hiyo kwenye mechi za mashindano
kutokana na kupata majeraha kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya
dhidi ya Namungo mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Avic Town Kigamboni.
Chanzo cha kuaminika kutoka kwenye uongozi
kilisema kwamba wachezaji hao ni muhimu kwa Yanga na wanafikiria lolote
linaweza kutokea kabla ya usajili wa Krisimasi. Wachezaji walioko kwenye hatari
ya kuwapisha Kambole na Yacouba kwenye dirisha hilo ni Lucapel Moloko na
Makambo ambao wanamulikwa kwa karibu sana na Nabi.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Saad
Kawemba, alisema ni lazima sheria ifuatwe hivyo wachezaji waliowasajili ni mali
ya Yanga Sc lakini kati yao hao 14 wawili watabaki kuwa mali ya timu na 12
wamesajiliwa.
“Wote waliopo ni mali ya klabu wataendelea kuwepo watahudumiwa na klabu na wataendelea kuwepo kikosini,”alisema Kawemba ambae aliwahi kuwa kiongozi wa TFF, Mtibwa na Azam kwa nyakati tofauti.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka Zaidi