AZAM FC imefikia makubaliano na Denis
Lavagne, kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa
mechi zake za nyumbani.
Kocha huyo raia wa Ufaransa ana leseni ya
juu ya ukocha (UEFA Pro Licence), anaibuka Azam FC kuchukua mikoba ya Abdihamid
Moallin.
Lavagne anatarajia kutua nchini leo
Jumanne, tayari kuanza rasmi majukumu yake hayo.
Moallin aliongoza timu hiyo msimu huu wa
2022/23 kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180.
Aliambulia ushindi kwenye mchezo mmoja
dhidi ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 na sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Geita
Gold.
Agosti 29 taarifa rasmi ilitolewa kutoka
Azam FC ikieleza kuwa imefikia makubaliano maalumu ya kuachana na kocha huyo
kwa upande wa majukumu ya kuwa kocha mkuu wa Azam FC atapangiwa majukumu
mengine.
Pia hata msaidizi wake Omary Nasser naye pia aliachia mamlaka hiyo ndani ya Azam FC.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka ZaidiDownload/Pakua App ya Timu ya Wananchi Google Playstore BOFYA HAPA
Tags
Usajili