Club ya Yanga Sc Jana
kwa kushirikiana na UNICEF wametangaza kuelekea mchezo wao wa Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain utakaochezwa November 02, 2022 katika
Uwanja wa Benjamin Mkapa watatoa elimu ya kuchanja kujikinga na maambukizi ya
UVIKO 19 pamoja na kutoa elimu kuhusu Ebola.
Katika zoezi hilo
ambalo Yanga Sc watazunguuka katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa
siku tano watatoa bure jumla ya tiketi za 10,000 kwa Mashabiki wao wataoshiriki
kupata elimu na kuchanja.
Taarifa hizo zimetolewa leo na CEO wa Yanga SC Andrew Mtine pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Jackson Group Kelvin Twissa ambao ni Washirika wa Yanga SC upande wa masoko.
"Tiketi za Zawadi
kwa Mashabiki ambao watachanja chanjo ya Uviko-19 zitapatikana kwenye maeneo
ambayo yatatangazwa kwenye mitandao ya Kijamii.
Katika maeneo hayo
kutakuwa na burudani mbalimbali na hakuna gharama za kuchanja" Mtendaji
Mkuu @jackson.group Kelvin Twissa
Download/Pakua App ya Timu ya Wananchi Google Playstore BOFYA HAPA
Tags
Habari