NASREDDINE Nabi, Kocha
Mkuu wa Timu ya Wananchi, Yanga Sc ameweka wazi kuwa mpango kazi namba moja ni
kuanza kupata ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club
Africain ya Tunisia.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Timu ya Wananchi App kwenye Simu Yako Upate Habari Za Timu yako Kwa Haraka Zaidi
Kesho Novemba 2, Yanga
Sc ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa mtoano kuwania kufuzu hatua
ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa kisha ule wa pili Yanga Sc itakuwa ugenini nchini Tunisia kukamilisha kete ya pili.
“Maandalizi yapo
vizuri na kila mchezaji anajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo na benchi la
ufundi linahitaji kuona tunapata kile ambacho tunastahili.
“Kuna kazi kubwa
inahitajika kufanyikakwa wachezaji ili kupata matokeo kwani kwenye hatua hizi
kila timu inaigia uwanjani ikiwa inajiamini na malengo ni kupata ushindi,”.
Nabi anafanya kazi kwa
ushirikiano na msaidizi wake Cedrick Kaze.
TAZAMA BAO LA USHINDI LA FISTON MAYELE DHIDI YA AZAM FC
Download/Pakua App ya Timu ya Wananchi Google Playstore BOFYA HAPA
Tags
Kimataifa