Wakati Yanga Sc ikirejea kutoka Mwanza ilipocheza mechi ya Ligi Kuu na kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, kocha Nasreedine Nabi amesema akili yao sasa ni jinsi gani watashinda mechi yao dhidi ya Club Africain ya Tunisia.
Timu ya Wananchi
itashuka kwenye Uwanja wa Mkapa, ikiikaribisha Club Africain, katika mchezo wa
kwanza wa hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza jana, Nabi
alisema anajua mchezo huo utakuwa mgumu, lakini mazoezi yao na maombi yake
yatakuwa katika wachezaji wake kucheza vyema kwenye kukaba watakapokuwa
wanashambuliwa.
Nabi alisema Yanga Sc inaweza
kushinda mechi hizo, lakini ushindi wake utatokana na jinsi itakavyopunguza
makosa ya kulinda kuanzia eneo la kiungo kwenda kwa mabeki wake.
“Hii ni mechi ngumu
(dhidi ya Club Africain), tunakwenda kukutana na timu ambayo inacheza kwa
utamaduni wa Watunisia, kupambana sana kwa nguvu, hii ni lazima tuwe na
mabadiliko makubwa katika nidhamu ya ukabaji na kuzuia kwenye eneo letu la
ulinzi.