Wakati siku tano zijazo Timu ya Wananchi, Yanga Sc itakuwa mjini Tunisia, Tunisia kuikabili Club Africain katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, timu hiyo imepewa mbinu za kuifunga miamba hiyo.
Wakati siku tano zijazo Yanga Sc itakuwa mjini Tunisia, Tunisia kuikabiri
Club Africain katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, timu
hiyo imepewa mbinu za kuifunga miamba hiyo.
Yanga Sc inahitaji
ushindi au sare ya mabao itakaporudiana na Club Africain, Novemba 9, ili
kutinga hatua ya makundi kwenye mashindano hayo baada ya juzi kulazimishwa
suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
ISOME NA HII >>Marudiano, Yanga Sc yawekewa Sh600 milioni mezani
Hata hivyo, timu hiyo
imeambiwa kama ikitulia ina uwezo wa kuwashangaza Watunisia hao ambao wanatajwa
kuwa na fujo na fitina za soka wakicheza nyumbani, ingawa pia inatajwa kupata
upinzani kwa baadhi ya mashabiki ikiwa kwao.
“Kama Yanga itajipanga
vizuri itaifunga, waache kuzifikiria fitina na fujo za wapinzani, wao wapambane
uwanjani kutafuta matokeo tu,” >>alisema nyota wa Kipanga, Abdillah
Suleiman Kombo ‘Mido Kubwa’ aliyekuwa miongoni mwa wachezaji waliofungwa na
timu hiyo nchini Tunisia.
Alisema ukiachana na
matokeo ya karibuni ya kimataifa, timu hiyo si tishio sana kwenye ligi yao,
huku akifichua kwamba Yanga Sc inachotakiwa ni kuidhibiti dakika 30 za kipindi
cha kwanza na ikiweza itangulie kufunga lakini wakianza kufungwa basi timu hiyo
itacheza hadi na waokota mipira.
“Wakiwa wanaongoza,
hata waokota mipira wanajichelewesha kuwapa mipira, pia mashabiki wao wana fujo
hadi za kurusha chupa uwanjani, lakini Yanga wala wasizingatie, ingawa kwenye usalama
askari wao wako vizuri.
ISOME NA HII >>"Bado Tuna nafasi Kimataifa" - MAYELE
“Vyumba vya
kubadilishia nguo pia hakuna shida na hata hotelini, kuna ulinzi, sisi
tulipokwenda askari wao walikuwa wengi na walitulinda kuhakikisha hatupati
tatizo kuanzia hotelini hadi tunaingia uwanjani,”>> alisema Mido Kubwa.
Akiwazungumzia ndani
ya uwanja, kiungo huyo alisema wana uwezo wa kuuchezea mpira na ukiwa kwa
wapinzani wanahakikisha wanakukabia golini kwenu hawakupi nafasi.