Fedha hizo ni kwa timu
itakayoingia makundi ya michuano hiyo, ingawa Yanga Sc italazimika kupambana
kiume na kupata angalau sare yoyote ya mabao katika mchezo huo utakaopigwa
Jumatano ijayo kuanza saa 1:00 usiku.
Katika mchezo huo,
Watunisia walikuwa wakijiangusha ovyo na kuwavaa wachezaji wa Yanga Sc kila
mara kutafuta faulo sambamba na kupaki basi, jambo lililowapa ugumu nyota wa
Yanga Sc kupenya kusaka mabao, licha ya kutengeneza nafasi kadhaa ambazo
hazikuwa na madhara makubwa.
ISOME NA HII >>"Bado Tuna nafasi Kimataifa" - MAYELE
Ni mchezo ambao wageni
walionekana kucheza kwa hesabu zaidi huku muda mwingi wakijaribu kupoteza muda
wakilinda matokeo hayo ambayo yanawaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Yanga Sc ambayo
ilionekana kutawala mchezo kwa muda mrefu, ilitengeneza nafasi chache ambazo
ilishindwa kuzitumia mfano ile ya dakika ya 70’ ambayo Fiston Mayele aliachia
shuti kali la mguu wa kulia lililookolewa na kipa wa Club Africain.
Kipindi cha kwanza
hakikuonekana kuwa na hatari nyingi kwa kila upande hasa kwa wageni ambao
walionekana kuwaachia Yanga Sc umiliki wa mpira kwa muda mrefu huku wao
wakijaza idadi kubwa ya wachezaji katika eneo la ulinzi.
Tofauti na matarajio
ya wengi, Yanga Sc haikuonekana kutumia faida hiyo ya wapinzani kucheza kwa
kujilinda ambapo ilitumia muda mwingi kupiga pasi za pembeni na za nyuma huku
mara kadhaa ikijaribu kupiga mipira ya juu ambayo iliokolewa vyema na Club
Africain.